# @paul_mchumi on Instagram

- **Type:** Image
- **Original URL:** https://www.instagram.com/p/DVjeBl-jJWr
- **Gondola URL:** https://gondola.cc/posts/63287394-paul-mchumi-instagram
- **Thumbnail:** https://img.gondola.cc/tr:w-,h-,fo-auto/postThumbnails/def7661d0b.jpg
- **Posted:** 2026-03-06T19:09:47.000+00:00
- **Account Owner:** Paul Chengula (@paul_mchumi) — https://gondola.cc/paul_mchumi

## Caption

Hivi ushawahi kufikiria kuwa hiyo kazi inayokuchelewesha kurudi nyumbani, inayokupa presha ya Deadlines, na kukuacha umechoka... ndiyo inayolipa bili zako zote?

Wengi wetu tunasema, "Hii kazi inanipa Stress sana, natamani kuacha!" Lakini ukweli ni kwamba: Kama unahisi kazi inakupa Stress, basi jaribu kuiacha uone jinsi Stress inavyoongezeka zaidi ukiwa huna Ajira.

Kwanini usicheze na chanzo chako cha mapato? ✍️

Kiuchumi, kanuni ni moja tu: Usifanye masihara na kazi uliyonayo sasa. 

Hata kama unahisi mazingira ni magumu, hiyo ndiyo inakufanya uwe na uhakika wa kula, kulala, na kusogeza maisha mbele.

Hapa kuna mambo matatu (3) ya kukumbuka kabla hujaamua "kuacha":

 👉Pambania Chako (Protect Your Hustle): Kila kazi ina changamoto zake. Stress ya ofisini ina dawa (mapumziko au mpango kazi), lakini stress ya Kukosa Hela haina dawa zaidi ya kupata hela yenyewe.

 👉Don't Quit Without a Plan: Usiache kazi kwa sababu ya hasira (Emotional Decision). Kama unataka kuondoka, hakikisha una Plan B au biashara nyingine inayoweza kusimama.

 👉Appreciation is Key: Chukulia hiyo kazi kama daraja. Iheshimu, ifanye kwa moyo, na ipe thamani. Usiichukulie poa (don't take it for granted).

Ushauri wa Bure👇

 Kabla hujasema "nimechoka," kumbuka mtaani kuna maelfu ya watu wenye sifa kama zako wanaitafuta hiyo nafasi kwa udi na uvumba. Be grateful, be smart!

IMEANDIKWA NA
Paul Chengula 
0714 260266

#TanzaniaJobs #Ajira #BusinessAdvice #Maisha #FinancialFreedom WorkEthic

## Stats

- **Views:** 0
- **Likes:** 9
- **Shares:** 0
- **Comments:** 2

## Tags

maisha, financialfreedom, tanzaniajobs, businessadvice, ajira

---
Copyright (c) Gondola