# @paul_mchumi on Instagram

- **Type:** Image
- **Original URL:** https://www.instagram.com/p/DW1nu8JjAqy
- **Gondola URL:** https://gondola.cc/posts/63287881-paul-mchumi-instagram
- **Thumbnail:** https://img.gondola.cc/tr:w-,h-,fo-auto/postThumbnails/68b0c83563.jpg
- **Posted:** 2026-04-07T16:52:21.000+00:00
- **Account Owner:** Paul Chengula (@paul_mchumi) — https://gondola.cc/paul_mchumi

## Caption

Najua ulikua hujui hizi 5 

1️⃣ Kutengeneza Maelekezo ya Kazi (SOPs)
Siri ya makampuni makubwa kama KFC au klabu kubwa za michezo ni mifumo, siyo watu pekee.

 SOP ni mwongozo wa maandishi unaomwambia mfanyakazi "Hivi ndivyo tunavyofanya kazi hapa."
Usiandike mambo magumu. Andika "Checklist" ya mambo ya kufanya asubuhi duka likifunguliwa, mchana, na wakati wa kufunga.

Mfano: Kama una duka la nguo, SOP inaweza kusema: "Kila asubuhi, piga deki, futa vioo, na panga nguo kulingana na rangi." Hii inazuia mfanyakazi kukaa tu na kusubiri uje umwambie cha kufanya.

2️⃣ Fundisha Kazi kwa Cross-Training
Hii mbinu inazuia biashara "kutekwa nyara" na mfanyakazi mmoja. 

Kama mfanyakazi mmoja ndiye pekee anayejua siri ya kupika au siri ya kutoa oda, huyo mtu akiondoka, biashara inakufa.

Badilishana majukumu (Job Rotation) angalau mara moja kwa mwezi. Mfanye mhasibu akae mapokezi kwa saa chache, na mpokea wateja ajifunze jinsi ya kuandika ripoti ya mauzo..

3️⃣ Toa Mamlaka ya Kufanya Maamuzi (Empowerment)
Wafanyakazi wengi Tanzania wanaogopa "Boss" kuliko wanavyoipenda biashara. 

Hii inawafanya wawe wazito kufanya maamuzi mpaka upatikane.
Wafundishe kanuni zako za kibiashara (Core Values). 

Badala ya kuwapa majibu, waulize: "Wewe ungekuwa bosi hapa, ungemtatulia vipi huyu mteja?" Ukiona anatoa jibu zuri, mpe ruhusa ya kufanya hivyo bila kukuuliza tena.

4️⃣ Shadowing: Mfundishe kwa Kumwonyesha
Kufundisha kwa vitendo (On-the-job training) ni bora kuliko kusema tu maneno. 

Shadowing inajenga uelewa wa kwanini unafanya maamuzi fulani.

Unapofanya maamuzi magumu, mueleze msaidizi wako kwanini umefanya hivyo. Kwa nini umechagua supplier A na siyo B? Kwa nini umemkatalia mteja huyu kukopa

5️⃣ Tumia Mifumo ya Kidijitali (Accountability)
Hata uwe na wafanyakazi waaminifu vipi, "Human nature" inaweza kubadilika. Mifumo inakupa amani ya roho (Peace of mind) kwa sababu kila kitu kina rekodi.

Tumia Apps za kusimamia mauzo (Inventory management). Hii itakusaidia kuona mzigo unapoingia na unapotoka. 

Pia, ripoti za kila siku kupitia WhatsApp group zinafanya kila mfanyakazi ajue kuwa unachungulia kinachoendelea..

IMEANDIKWA NA
Paul Chengula (Mchumi)
0714 260266

#biashara #uchumi

## Stats

- **Views:** 0
- **Likes:** 4
- **Shares:** 0
- **Comments:** 2

## Tags

biashara, uchumi

---
Copyright (c) Gondola