# @paul_mchumi on Instagram

- **Type:** Image
- **Original URL:** https://www.instagram.com/p/DUbPwzHjGa7
- **Gondola URL:** https://gondola.cc/posts/63288377-paul-mchumi-instagram
- **Thumbnail:** https://img.gondola.cc/tr:w-,h-,fo-auto/postThumbnails/69d1df9bdf.jpg
- **Posted:** 2026-02-06T17:59:48.000+00:00
- **Account Owner:** Paul Chengula (@paul_mchumi) — https://gondola.cc/paul_mchumi

## Caption

Je, unajua kuwa mteja uliyenaye sasa hivi ndiye aliyebeba ufunguo wa faida yako kubwa? 🔑

Watu wengi wanahangaika kutafuta wateja wapya kila siku, lakini wanasahau mbinu moja ya dhahabu inayoitwa Cross-Selling.

Cross-Selling ni nini hasa?
Hii ni mbinu ya kumshawishi mteja anunue bidhaa nyingine ya ziada inayofanana au kusaidiana na ile aliyochagua tayari. 

Si kwamba unamlazimisha, bali unamsaidia kupata suluhisho kamili!

Tazama mifano hii 👇🏻
✅Unauza Simu: Mteja akinunua simu, mshauri achukue na Cover au Screen Protector ili kulinda simu yake mpya.

 ✅Kwenye Mavazi: Mteja akinunua suti, mpe elimu kwanini anahitaji tai au soksi nzuri za rangi inayoendana.

✅ Kwenye Chakula: Mteja akiagiza chakula,mshawishi anunue na maji au soda toka kwako

Kwanini Mbinu Hii Inalipa?
 👉🏻Inajenga Imani: Mteja anaona unamjali na unajua unachofanya, siyo tu unauza.

 👉🏻Inapunguza Gharama: Ni rahisi kumuuzia mteja aliyeko dukani kuliko kuanza kutafuta mteja mpya mtandaoni.

 👉🏻 Inaongeza Mauzo (Turnover): Badala ya kupata 50,000/= kwa mteja mmoja, unaweza kuishia kupata 70,000/= kwa kumuuzia bidhaa ndogo za ziada.

✍️Usiuze tu bidhaa, uza suluhisho! Elimisha mteja wako, mpe sababu kwanini hiyo bidhaa ya ziada ni muhimu kwake leo.

Paul Chengula 
📞
Piga/WhatsApp: 0714260266

#Biashara #Ujasiriamali #Tanzania #Mauzo #CrossSelling #ElimuYaBiashara #MbinuZaBiashara

## Stats

- **Views:** 0
- **Likes:** 5
- **Shares:** 0
- **Comments:** 0

## Tags

mbinuzabiashara, mauzo, tanzania, elimuyabiashara, biashara, ujasiriamali, crossselling

---
Copyright (c) Gondola