facebook pixel
Umewahi kujiuliza kwanini kadiri unavyopata mshahara mkubwa au faida zaidi kwenye biashara, ndivyo unavyozidi kuishiwa mapema? Jibu haliko kwenye kiasi unachoingiza, bali liko kwenye Nidhamu yako ya Kihisia (Emotional Discipline). Katika ulimwengu wa uchumi, usimamizi wa fedha ni 20% tu maarifa ya kichwani, lakini 80% ni tabia zako za kila siku. Mtego wa "Lifestyle Creep" Wengi wetu tukiingiza fedha zaidi, tunahisi ni lazima tubadilishe maisha ili "kuendana na hadhi". Hapa ndipo tunapoanza kununua vitu ili tuwafurahisha watu ambao hata hawajali maisha yetu. BAJETI SIO KIFUNGO NI TAA Watu wengi wanaogopa kupanga bajeti wakidhani inawabana wasitumie pesa zao. Ukweli ni kwamba, bajeti ni kama taa inayokuonesha wapi pesa yako inatakiwa kwenda badala ya kuishangaa inapotea kizembe. Hatua za Kuchukua Leo: 👉🏻Funga Akili Kabla ya Pochi: Usifanye matumizi kwa mihemko au sifa. Jiulize, "Je, ninanunua hiki kwa sababu nakihitaji au kwa sababu nataka nionekane nina uwezo?" 👉🏻Jifunze...

 7

    Suggested Credits
    Tags, Events, and Projects